Pata taarifa kuu
JAPAN-TAIWAN-CHINA

Meli za Japan zakabiliana na mamia ya boti za wavuvi wa Taiwan walioingia kwenye visiwa vya Senkaku

Meli za usalama za Japan zimetumia maji ya kuwasha kukabiliana na mamia ya boti za wavuvi wa Taiwan walioingia kwenye visiwa vya Senkaku ambavyo vinagombewa na nchi za Japan na China.

Baadhi ya meli za wavuvi wa Taiwani wakiingia kwenye eneo la visiwa vya Senkaku
Baadhi ya meli za wavuvi wa Taiwani wakiingia kwenye eneo la visiwa vya Senkaku REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilitokea wakati ambapo meli za Japan zilipowataka wavuvi hao kuondoka kwenye eneo la visiwa hivyo ambavyo inadai ni mali yake lakini wavuvi wa Taiwan waligoma na kuendelea kusalia kwenye eneo hilo ndipo walipoanza kurushiana maji ya kuwasha.

Wavuvi hao ambao nao walikuwa na Meli kubwa zenye maji ya kuwasha walianza kujibizana na zile za Japan na tukio hilo kudumu kwa zaidi ya saa mbili.

Hii ni mara ya kwanza kwa wavuvi wa Taiwan kuingia kwenye eneo la visiwa hivyo ambavyo nayo inadai umiliki halali ambapo Serikali ya nchi hiyo hivi karibu ilitangaza kudai umiliki wa visiwa hivyo.

Katibu wa baraza la mawaziri nchini Japan, Osamu Fujimura amethibitisha Meli zake kutumia maji ya kuwasha kuwarudisha nyuma wavuvi hao jaribio ambalo amesema lilifanikiwa.

Katika hatua nyingine Serikali ya Japan imeituhumu Serikali ya China kuichokoza nchi yake kwa kupeleka meli za kijeshi kwenye eneo hilo ambalo bado linamgogoro huku nchi zote mbili zikiendelea kusisitiza kuwa na umiliki halali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.