Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/04 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/04 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/04 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Serikali ya Syria yakataa ripoti ya UNICEF inayoonesha ukiukwaji wa haki za watoto katika Taifa hilo

media Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa UN Bashar Jaafari akihutubia Mkutano wa Umoja huo

Serikali ya Syria imekataa ripoti ya Umoja wa Mataifa UN iliyowasilishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Usalama inayoonesha unyanyasaji wanaoufanywa dhidi ya watoto katika kipindi cha miezi kumi na minane ya machafuko. Balozi wa Syria kwenye Umoja wa Mataifa Bashar Jaafari amepinga vikali ripoti hiyo ambayo imetolewa na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF ikionesha vitendo vya uhalifu vinavyofanywa dhidi ya watoto.

Ripoti hiyo imeeleza kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto nchini Syria ikiwemo mauaji dhidi ya kundi hilo ambao umekuwa ukifanywa na vikosi vya serikali ya Rais Bashar Al Assad.

Balozi Jaafari amesema hizo ni propaganda ambazo zimekuwa zikiandaliwa na mataifa ya magharibi kwa lengo la kuonesha duniani jeshi la serikali ya nchi hiyo ndiyo limekuwa likitenda vitendo viovu kitu ambacho si cha kweli.

Balozi Jaafar ameuambia mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni wapiganaji wa Jeshi Huru la Syria ndilo ambalo limekuwa likiajiri hadi watoto kwenye jeshi lake na ndiyo wanakiuka haki za watoto.

Mwakilishi huyo wa Syria katika Umoja wa Mataifa amekosoa ripoti hiyo na kusema haina ushahidi wowote wa maana ambayo unaweza ukathibitisha serikali ya Rais Assad imekuwa ikitenda vitendo vya ukiukwaji wa haki za watoto.

UNICEF kwenye ripoti hiyo imeonesha mashambulizi ambayo yamefanyika nchini Syria kwa miezi kumi na nane yamesababisha kuharibiwa kwa shule zaidi ya elfu ishrini na sita kitu ambacho kinadhihirisha uhalifu dhidi yao.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama ametaka watoto walindwe kwenye sehemu za vita huku akiepuka kuitaja moja kwa moja nchi ya Syria.

Machafuko ya Syria ya miezi kumi na nane yamesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu ishrini na tisa kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa UN.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana