Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Kundi la M23 lakanusha tuhuma katika ripoti ya Human Rights Watch kuhusu kutekeleza mauaji ya kivita

media Mwanamama mkimbizi akiwa na mwane mgongoni mbele ya wapiganajiwa M23 kaskazini mwsa Mkoa wa Kivu Julai 26, 2012. AFP PHOTO/PHIL MOORE

Kundi la Waasi la M23 linalopambana na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Mashariki mwa Taifa hilo limetuhumiwa kuhusika na mauaji ya raia sambamba na makosa ya kivita katika ripoti iliotolewa na Shirika la kimatiafa linalo tetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch.

Shirika la Kutetea Haki za BinadamuHuman Rights Watch limesema Kundi la M23 limeendelea kutekeleza mauaji ya watu wasio na hatia pamoja na kuendelea kuajiri watoto wadogo na kuwauwa vijana wanaopinga kujiunga na kundi hilo, vitu ambavyo vinakwenda kinyume na sheria za kimataifa.

Kwa mujibu wa Anneke Van Woundenberg wa Human Rights Watch tawi la Afrika amesema ripoti hiyo imetolewa baada ya uchunguzi wa kina uliofanyika kati ya mwezi Mei na Septemba mwaka huu ambapo takriban watu zaidi ya 190 walihojiwa.

Miongoni mwa watu waliohojiwa katika uchunguzi huo ni pamoja na waathirika wa vita hivyo raia wa Congo na wa Rwanda, wajumbe wa familia za waathirika, mashahidi, viongozi mbalimbali wa vijiji pamoja na wapiganaji zamani wa kundi la M23.

Anneke Van Woundenberg amesema hata viongozi wa Rwanda wanaweza kuchukuliwa kama washirika wa mauaji hayo kwa kuwapa msaada wa kijeshi wapiganaji wa kundi la M23. Jambo ambalo vingozi wa Rwanda wanaendelea kukanusha

Kiongozi huyo wa Human Rights Watch tawi la Afrika amesema kwamba ni muhimu kwa kipindi hiki wafadhili wa Rwanda kuchunguza mdaada unaopewa kwa nchi hiyo iwapo hauchangii kuchochea machafuko mashariki mwa DRCongo.

Mwenyekiti wa kundi la M23 Jean Marie Runiga ametupilia mbali tuhuma hizo huku akisisitiza kuwa M23 haijawahi kupewa msaada wowote kutoka ugenini, na kwamba hawajawahi kutekeleza mauaji yoyote, vijana wanaoajiriwa katika kundi hilo wanakuja kwa khiari yao, na iwapo kuna mpigananii wa M23 ataehusika na tukio hilo atahukumiwa kwa mujibu wa sheria.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana