Pata taarifa kuu
Syria-mapigano

Ban Ki Moon ataka wahusika wa mauji nchini Syria wahukumiwe, wakati mkutano wa pande nne kuhusu Syria ukizinduliwa jijini Kairo

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amelimbia baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuwa wahusika wa mauaji ya kivita nchini Syria lazima wahukumiwe. Akizungumza mbele ya washiriki kutoka nchini 47 katika mkutano wa wiki tatu jijini Geneva nchini Uswisi, Ban Ki Moon amesema kuwa Umoja wa Mataifa utahakikisha wahusika wote wa mauaji ya kivita kutoka pande zote mbili zinazozozana nchini Syria wanafikishwa mahakamani.

Lakhdar Brahimi (G), mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za kiarabu kuhusu Syria, akiwa na Ban Ki Moon, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Agosti 24, 2012.
Lakhdar Brahimi (G), mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za kiarabu kuhusu Syria, akiwa na Ban Ki Moon, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Agosti 24, 2012. REUTERS/J.C. McIlwaine/UN Photo/Handout
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe katika kikao hicho za baraza la haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa wanagusia mzozo wa Syria unaendelea sasa ni zaidi ya mwaka mmoja.

Hayo yanajiri wakati msuluhishi wa mgogoro wa Syria, Lakhtar Brahimi ameanza ziara nchini Misri katika kazi ngumu na nzito ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa Syria siku moja baada ya kutokea mlipuko mkubwa katika mji wa Allepo unaoendelea kushuhudia machafuko makubwa ikiwa ni wiki ya saba sasa.

Wakati huo huo serikali ya Iran imetangaza kwamba itashiriki jumatatu katika mkutano wa kwanza wa kundi la pande nne kuhusu Syria ambao ulipendekezwa na Misri. Maofisa kadhaa wa serikali ya Iran wamenukuliwa na kituo cha Iran cha Al Alam idhaa ya Kiarabu wakithibitisha.

Naibu Waziri wa mambo ya Nje Hossein Amir Abdollahian atashiriki mkutano jijini Kairo utaozikutanisha pande nne, ikiwa ni pamoja na Misri, Iran, Saudi Arabia na Uturuki, uliopendekezwa na rais wa Misri Mohamed Morsi ili kutatua mgogoro wa Syria viongozi wa Iran wametbitisha kupitia kituo cha habari cha Al Alam.

Ushiriki wa Iran katika mkutano huu ni sehemu ya jitihada za kutatua mgogoro wa Syria na itaruhusu kusikiliza mapendekezo Misri," alisema Msemaji wa Wizara ya Nje wa Iran Ramin Mehmanparast alinukuliwa na Al Alam.

“Serikali ya Iran itachangamkia fursa hii kueleza nafasi yake, ikiwa ni pamoja na nia yake ya kupanua kundi hili kwa nchi nyingine," aliongeza.

Hata hivyo hakutowa maelezo zaidi, lakini mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge, la Iran, Alaeddin Boroujerdi, aliiambia Al-Alam kwamba Tehran inataka kujumuisha Iraq katika kundi hilo lililopendekezwa Agosti mwaka huu na rais Morsi katika mkutano wa kilele wa Shirika la Kiislam (OIC) katika mji wa Makkah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.