Pata taarifa kuu
MAREKANI -GAMBIA

Marekani yaitaka Gambia kufuta adhabu ya kifo kwa wafungwa

Marekani imeitaka Gambia kuachana na mpango wake wa kutoa adhabu ya kifo dhidi ya wafungwa wake, na kukemea ukosefu wa uwazi baada ya rais wa Gambia, Yahya Jameh kuwahukumu kifo wafungwa tisa adhabu iliyotekelezwa kwa kufyatuliwa risasi.

Victoria Nuland, msemaji wa Ikulu ya Marekani ambayo imetoa kalipio kwa raisi wa Gambia kuacha adhabu ya kifo kwa wafungwa
Victoria Nuland, msemaji wa Ikulu ya Marekani ambayo imetoa kalipio kwa raisi wa Gambia kuacha adhabu ya kifo kwa wafungwa AFP PHOTO/MASSOUD Hossaini
Matangazo ya kibiashara

Wito huo kwa rais wa Gambia umetolewa na msemaji wa Ikulu ya Marekani, Victoria Nuland ambaye amemweleza raisi Jammeh kuachana na mpango huo mara moja na kurejea tena katika kushughulikia Kesi nchini humo.

Nuland ametoa wito kwa Gambia kuhakikisha kuwa Kesi zote zinashughulikiwa kwa Mujibu wa sheria za nchi hiyo halikadhalika kwa kufuata wajibu wa kimataifa.

Jammeh Mwanajeshi wa zamani nchini Gambia aliyeingia madarakani baada ya mapinduzi mwaka 1994, alitoa amri ya kuuawa kwa wafungwa tisa kwa kupigwa risasi na kuahidi kutoa hukumu ya kifo kwa wafungwa wengine 38 ifikapo katikati ya mwezi ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.