Pata taarifa kuu
Pakistani-Marekani

Marekani yapuuza kauli ya Assange, yasifu Pakistan kuchunguza aliyechoma Quran

Serikali ya Marekani kupitia wizara ya mambo ya nchi za nje imekanusha vikali kauli iliyotolewa na mmiliki wa mtandao wa wikileaks Julian Assange kuwa nchi hiyo inatafuta mchawi wake kupitia mtandao wake.

REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa wizara hiyo Victoria Nuland amesema kuwa nchi yake haina mkono wowote kuhusu Assange kuhamishiwa nchini Sweeden na baadae kupelekwa nchini humo na kwamba matamshi yake hayana tija.

Katika hatua nyingine Rais wa Ecuador Rafael Correa ambaye nchi yake kupitia ubalozi wake wa jini London Uingereza ulikubali kumpatia Assange hifadhi ya kisiasa Assange, ameendelea kutetea uamuzi wake na kuahidi kutomkabidhi Assange kwa mamlaka nchini humo mpaka pale watakapohakikishiwa usalama wake.

Wakati huohuo ikiwa ni siku moja imepita toka rais wa Pakistan Asif Ali zardari aagize polisi kuchunguza kesi dhidi ya msichana anayetuhumiwa kuchoma kitabu cha Quran, serikali ya Marekani imepongeza hatua hiyo ingawa bado inawasiwasi kuhusu msichana huyo kutendewa haki.

Msichana huyo mkristo anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili, alikamatwa juma lililopita nyumbani kwao baada ya majirani kuripoti polisi kuwa alikuwa akichoma moto kitabu kitakatifu cha Quran.

Rimsha ameendelea kuwekwa kizuizini chini ya ulinzi mkali wa polisi ambapo kwa mujibu wa sheria za Pakistan endapo msichana huyo atapatikana na hatia basi atakabiliwa na adhabu ya kifo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.