Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI

Marekani yathibitisha mabalozi wawili kuasi Syria

Wakati huohuo Marekani imethibitisha kuwa mabalozi wawili wa Syria katika Umoja wa Falme za Kiarabu na Cyprus wameasi utawala wa Syria na wameelezea hatua kama mafanikio kwao.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jay Carney amasema kuwa kuasi kwa mabalozi hao ni ishara kuwa viongozi waandamizi katika utawala wa Bashar Al Assad hawakubaliani na kile utawala huo unakifanya na kusababisha mauaji ya raia.

Amesema kuwa hatua hiyo inaashiria kuwa siku za utawala wa Assad zinahesabika na kuicha nchi hiyo ikingia katika mkondo wa kusaka demokrasia.

Wakati huohuo mapigano zaidi yameripotiwa kwenye miji mikubwa mitatu nchini Syria ambapo wanajeshi wa Serikali wamezidisha mashambulizi dhidi ya waasi wa nchi hiyo waliokuwa wanashikilia baadhi ya maeneo.

Makabiliano makubwa yameripotiwa kwenye miji ya Allepo, seheumu ya vitongoji vya Damascus na sasa kwenye eneo la Al-Rastan ndani ya mji wa Homs na kuendelea kuzusha hofu kwa raia.

Mkuu mpya wa msafara wa waangalizi wa Umoja wa mataifa nchini humo Luteni Jenerali Babacar Gaye amesema kuwa wamerejea wakiwa na nguvu mpya na wana imani kuwa mapigano yanayoendelea yatasitishwa.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameendelea kusisitiza kwa jumuiya ya kimataifa kutokukaa kimya kuzua vifo vinavyoendelea kushuhudiwa nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.