Pata taarifa kuu
Kenya

Wanariadha Kenya waapa kuvunja rekodi michezo ya Olimpiki

Bingwa wa dunia wa mbio za mita 1500 Asbel Kiprop kutoka Kenya ameelezea matumaini yake kuwa Kenya itavunja rekodi iliyowekwa na Noah Ngeny miaka 12 iliyopita katika mashindano ya Olimpiki yanayotarajiwa kuanza ijumaa wiki.

Matangazo ya kibiashara

Kiprop akishirikiana na wanariadha wenzake kutoka Kenya Silas Kiplagat na Nixon Chepseba wanaunda timu ambayo itakuwa tishio katika mashindano hayo kwa kuwa wote wameonyesha kukimbia kwa kasi zaidi katika mashindano mbalimbali duniani mwaka huu.

Amesema kuwa ni vigumu kwake kutabiri nani atatoka na medali ya dhahabu kati wanariadha hao watatu lakini anaamini kuwa rekodi hiyo ya Noah Ngeny ya kutumia dakika 3 na sekunde 29.77 itavunjwa.

Mwanariadha huyo amesema wako tayari kushiriki na kufanya vizuri katika mashindano hayo ya Olimpiki yanayofanyika London nchini Uingereza na wameapa watanfanya maajabu.

Kiprop amefahamisha kuwa zitakuwa ni mbio zenye ushindani lakini ana uhakika watapeleka medali tatu za mbio hizo nchini Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.