Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Daktari wa Pakistan aliyesaidia kuuawa kwa Osama Bin Laden afungwa jela miaka 33

Daktari wa zamani wa serikali ya Pakistani Shakeel Afridi ambaye aliwasaidia Majasusi wa Marekani CIA kumuua Kiongozi wa Mtandao wa Al Qaeda Duniani Osama Bin Laden amehukumiwa kifungo cha miaka thelathini na tatu kwa kosa la uhaini.Afridi ambaye ni mtaalam wa upasuaji amehukumiwa kwa mujibu wa sheria za kikabila za eneo la Khyber pamoja na kulimwa faini ya dola elfu tatu na mia tano kosa likiwa uhaini na tayari ameshapelekwa Peshawar kutumikia kifungo chake. 

RFI
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Utawala wa Khyber Mohammad Siddiq amethibitisha kufungwa kwa Daktari Afridi wakisema kitendo chake cha kufanya uchunguzi wa vinasaba kubaini kama aliyeuawa alikuwa Osama Bin Laden lilikuwa kosa la kihaini.

Pamoja kifungo na faini hiyo ya dola za kimarekani 3,500, daktari huyo alipewa hukumu hiyo bila ya yeye kuwepo mahakani na amefanya kazi ya udaktari kwa kipindi kirefu akijihusisha na upasuaji.

Katika hatua nyingine daktari huyo hakupewa nafasi ya kujitetea kutokana na tuhuma hizo na kulingana na taratibu za kabila hilo asingeweza kuwa na uwezo kumpata mwanasheria wa kumtetea.

Mwezi Januari, waziri wa ulinzi wa Marekani Leon Panetta alithibisha kuwa Afridi alifanya kazi na maafisa usala wa taifa la Marekani akikusanya vipimo vya Vinasaba, DNA ili kutambua uwepo wa Osama Bin Laden nchini Pakistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.