Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA

Mahakama kuu ya Israel yatupa rufaa ya wafungwa wawili wakipalestina walio kwenye mgomo kula

Mahakama kuu nchini Israel imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na wafungwa wawili wakipalestina ambao wako kwenye mgomo wakula kupinga kuendelea kuwekwa kizuizini bila ya mashtaka na polisi nchini humo.

Baadhi ya raia wakipalestina wakiwa na mabango yanayowaonesha wafungwa ambao wako kwenye mgomo wakitaka waachiliwe huru
Baadhi ya raia wakipalestina wakiwa na mabango yanayowaonesha wafungwa ambao wako kwenye mgomo wakitaka waachiliwe huru Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wafungwa hao Bilal Biab na Thaer Halahleh wamekuwa kwenye mgomo wa kutokula kwa muda wa siku 70 ambapo wamekuwa wakishinikiza kuachiliwa huru na mamlaka za Israel kwakuwa mpaka sasa hawajasomewa mashtaka yao.

Wanaharakati wa haki za binadamu wakiongozwa na wanasheria wa wafungwa hao, walikata rufaa kwenye mahakama kuu ya nchi hiyo wakitaka wafungwa hao kuachiliwa huru kwa dhamana wakati wakisubiri kesi yao.

Awali wafungwa hao walihukumiwa kwenda jela bila ya kusomewa mashtaka kwakile kilichoelezwa kuwa uchunguzi wao unaendelea na hivyo kwa usalama wa nchi hiyo ni lazima washikiliwe chini ya ulinzi mkali.

Wanasheria wa wafungwa hao, mara baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, wamewaambia waandishi wa habari kuwa kulingana na uamuzi wa mahakama kuu ni wazi Serikali imedhamiria kuwanyima haki wafungwa hao kwakuruhusu kuendelea kushikiliwa kinyume na sheria na mkataba wa haki za binadamu.

Hata hivyo mahakama hiyo imeamuru polisi kuhakikisha wafungwa hao wanapatiwa huduma za kimatibabu kwa wakati hasa wakati huu ambapo wanaendelea na mgomo wao wakutokula.

Wafungwa hao wawili ni kati ya maelfu ya wafungwa wengine wakipalestina ambao wanashikiliwa kwenye magereza ya nchini Israel ambao wanafikia elfu 2500 wakiwa wanashiriki mgogmo wakutokula kwa karibu siku 19 sasa kupinga wenzao kunyanyaswa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.