Pata taarifa kuu
CAMBODIA

Viongozi wa zamani wa kundi la Khmer Rouge nchini Cambodia wapandishwa kizimbani

Kesi dhidi ya viongozi wanne wa kundi la Khmer Rouge waliongoza chama cha Kikomunisti nchini Cambodia kati ya mwaka 1975 hadi 1979,wakati wa uongozi wao ambao kulitokea mauji ya halaikii ya watu zaidi ya Milioni mbili raia wa Cambodia.

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Cambodia wakati wa utawala wa Khmer Rouge, Ieng Sary akiwa mahakamani
Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Cambodia wakati wa utawala wa Khmer Rouge, Ieng Sary akiwa mahakamani Reuters路透社
Matangazo ya kibiashara

Washukiwa hao wamepinga tuhuma za kuhusika katika mauji hayo makubwa katika historia ya nchi hiyo,huku kesi dhidi yao ikitazamiwa huenda ikachukua miaka minne hadi kukamilika.

Mwaka uliopita,mmoja wa viongozi wa zamani wa kundi hilo Kaing Guek Eav, aliyefahamika kwa jina lingine kama Copmrade alifungwa jela miaka 35 baada ya kubainika kuwa alihusika na mauji hayo pamoja na visa vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kesi hiyo ambayo imenza kusikilizwa leo asubuhi inaongozwa na umoja wa mataifa UN jijini Phnom huko Cambodia,inawahusisha Nuon Chea,rais wa zamani Khieu Samphan, na mawaziri wa zamani Ieng Sary na Ieng Thirith.

Washukiwa wote wanne wanakabiliwa na mashtaka zaidi ya kumi ikiwemo uhalifu wa kivita, ukiukaji wa haki za binadamu, mauaji ya halaiki pamoja na uchochezi wa kidini ambapo washukiwa wote wanne isipikuwa mmoja wameonesha kutotaka kushirikiana na mahakama inayosikiliza kesi hiyo.

Washukiwa hao wanatarajiwa kufikishwa tena katika mahakama hiyo, baadaye mwezi Septemba mwaka huuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.