Pata taarifa kuu
Soka Barani Afrika-AFCON 2015

Afcon 2015: DRC yaburuzwa kwa mabao 3-1

Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo imepata pigo kubwa baada ya kuburuzwa na Cote d'Ivoire katika michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika nchini Equatorial Guinea.

Gervinho anafurahia bao lake akiwa pamoja na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Cote d'Ivoire dhidi ya DRC. Cote d'Ivoire imetinga fainali ya Afcon 2015.
Gervinho anafurahia bao lake akiwa pamoja na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Cote d'Ivoire dhidi ya DRC. Cote d'Ivoire imetinga fainali ya Afcon 2015. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Usiku wa Jumatano Februari 4 kuamkia Alhamisi Februari 5 ulikuwa mgumu kwa wananchi na mashabiki wa soka wa timu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya kufungwa na Cote Dvoire mabao 3 kwa 1 katika mchuano wa nusu fainali, kutafuta ubingwa wa Afrika.

Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa Bata nchini Equaitorial Guinea.

Cote d'Ivoire ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 20 ya mchuano huo kupitia nahodha Yaya Toure, baada ya kupiga mkwaju wa nguvu kutoka mita 20 na lango la DRC na kutikisa nyavu.

Dakika nne baadaye, DRC walisawazisha baada ya kupata penalti iliyotiwa kimyani na Mbokani Bezua, baada ya beki wa Cote d'Ivoire, Eric Bailly, kuunawa mpira katika eneo la hatari.

Mshambualiji Gervihno aliiongezea Cote d'Ivoire bao la pili katika dakika ya 41, kabla ya kipindi cha mapumziko, na baadaye  Wilfried Kanon kuihakikishia vijana wa kocha Hervé Renard ushindi na kufuzu katika hatua ya fainali.

Cote d'voire sasa inasubiri mshindi wa mechi ya nusu fainali ya leo kati ya Ghana na wenyeji Equitorial Guinea, kufahamu ni nchi ipi itakayomenyana nayo wakati wa mechi ya fainali siku ya Jumapili Februari 8 mwaka 2015.

Cote d' Ivoire mara ya mwisho kushinda taji hili la Afrika ilikuwa ni mwaka 1992 lakini mwaka 2006 na 2012 walifika fainali na kufungwa.

Leopard ya DRC sasa itacheza siku ya Jumamosi Februari 7 kutafuta nafasi ya tatu na timu itakayopoteza leo Alhamisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.