sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Matukio tuliyoyapa uzito wiki hii duniani
Rais wa DRC Felix Tshisekedi
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
CAN 2015

Afcon 2015: DRC yajiandaa kumenyana na Cote d'Ivoire

media Mchezaji wa Equatorial Guinea, Javier Balboa, mchezaji wa DRC, Jeremy Bokila, mchezaji wa Cote d'Ivoire, Yaya Toure na mchezaji wa Ghana Asamoah Gyan (kuanzia kushoto kwenda kulia). REUTERS/Hutchings & Abdallah Dalsh - AFP / DE SOUZA –Montage RFI

Leo ni siku ya maandalizi ya timu za taifa za soka za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Cote d'Ivoire kujiandaa kwa mchuano wa nusu fainali, kuwania taji la ubingwa wa Afrika.

Mechi hiyo itachezwa Jumatano Februari 4 katika uwanja wa Bata nchini Equatorial Guinea kuanzia saa nne usiku saa za Afrika Maashariki sawa na saa tatu usiku saa za Afrika ya Kati.

Mataifa haya mawili yalimenyana mwaka uliopita katika mechi ya kufuzu kucheza fainali hizi, DRC walifungwa mabao 2 kwa 1 nyumbani na walipokwenda Abidjan waliwafunga Cote d'Ivoire mabao 4 kwa 3.

Hii ni wazi kuwa mechi haitakuwa rahisi Jumatano wiki hii, na kocha wa Leopard Florent Ibenge atakuwa anataka kudhirihisha kuwa ana uwezo wa kuiongoza timu yake kufika fainali, sawa na Mfaransa Herve Renard ambaye lengo lake ni kuhakikisha kuwa Cote d'Ivoire inanyakua taji hilo walilonyakua mwisho mwaka 1992.

Nusu fainali ya pili itakuwa siku ya Alhamisi kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea katika uwanja wa Malabo.
Mshambualiaji wa Ghana, Asamoah Gyan anauguza jeraha.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana