Pata taarifa kuu
Soka Barani Afrika-AFCON 2015

Cote d'Ivoire na Ghana zafuzu katika robo fainali

Timu ya taifa ya soka ya Cote d'Ivoire na ile ya Ghana zimefuzu katika hatua ya nusu fainali kuwania ubingwa wa Afrika, baada ya kupata ushindi jana usiku katika michuano inayoendela nchini Equitorial Guinea.

Wachezaji wa Ghana washerehekea bao lililowekwa kimyani na Christian Atsu dhidi ya Guinea.
Wachezaji wa Ghana washerehekea bao lililowekwa kimyani na Christian Atsu dhidi ya Guinea. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji mpya wa Manchester City Wilfried Bonny aliifungia Cote d'Ivoire mabao 2, huku kabla ya Gervihno kufunga la tatu katika dakika tisini ya mchuano huo .

Cote d'Ivoire ndiyo iliyoanza kupata bao katika dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza kabla ya El Arbi Soudani kuishawazishia Algeria katika dakika ya 51, na baadaye Cote d'ivoire kufanikiwa kupata ushindi.

Cote d'Ivoire sasa itamenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mechi ya nusu fainali ya kwanza siku ya Jumatano Februari 4 katika uwanja wa Bata.

Black Stars ya Ghana nayo ilifuzu baada ya kuifunga Guinea mabao 3 kwa 0.

Mabao ya Ghana yalitiwa kimyani na Christian Atsu aliyefunga mabao mawili na Kwesi Appiah bao moja.

Ghana itamenyana na wenyeji Equitorial Guinea siku ya Alhamisi juma hili katika uwanja wa Malabo.

Equitorial Guinea waliweka historia kwa kufuzu baada ya kuishinda Tunisia mabao 2 kwa 1.

Fainali itachezwa siku ya Jumapili katika uwanja wa Bata.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.