Pata taarifa kuu
KENYA-MICHEZO-RIADHA

Dennis Kimetto avunja rekodi ya dunia mwaka 2014

Katika mchezo wa Riadha, kitakachokumbukwa mwaka huu ni kuvunjwa kwa Rekodi ya dunia katika mbio za Marathon iliyovunjwa na Mkenya Dennis Kimetto wakati wa mashindano ya Berlin Marathon nchini Ujerumani tarehe 28 mwezi wa Septemba.

Mkenya Dennis Kimetto avunja rekodi ya dunia mwaka 2014
Mkenya Dennis Kimetto avunja rekodi ya dunia mwaka 2014 REUTERS/Hannibal Hanschke
Matangazo ya kibiashara

Kimetto mwenye umri wa miaka 30, alivunja rekodi hiyo ya dunia kwa kumaliza mbio hizo kwa muda wa saa 2 dakika 2 na sekunde 57 na kuwa mwanaridha wa kwanza kuwahi kukimbia mbio za Marathon chini ya saa mbili na dakika 3.

Vile vile katika mchezo wa Riadha, itakumbukwa kesi ya mwanariadha mlemavu kutoka Afrika Kusini Oscar Pistorius, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka mitano baada ya kupatikana na kosa la kumuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Hata hivyo kesi ya mwanariadha huyo wa zamani ilirejeshwa Mahakamani kufuatia ombi la Ofisi ya mwendesha mashitaka.

Siku ya mwisho ya kusikilizwa kesi ya Oscar Pistorius, ambapo Mwendesha mashataka aliomba kifungo cha miaka 10 dhidi ya mwanariadha huyo mlemavu, Oktoba 17 mwaka 2014.
Siku ya mwisho ya kusikilizwa kesi ya Oscar Pistorius, ambapo Mwendesha mashataka aliomba kifungo cha miaka 10 dhidi ya mwanariadha huyo mlemavu, Oktoba 17 mwaka 2014. REUTERS/Werner Beukes/Pool

Desemba 10 mwaka 2014, jaji aliruhusu kesi hiyo isikilizwe katika kitengo cha rufaa, baada ya viongozi wa Mashitaka kukata rufaa kwa hukumu aliyopewa Oscar Pistorius.

Baada ya miezi minane kesi yake ikisikilizwa, Oscar Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp mwezi Februari mwaka 2013. Hukumu ambayo Ofisi ya Mashitaka haikukubaliana nayo.

Majaji walimkuta Oscar Pistorius na kosa la kuua bila kukusudia, lakini Ofisi ya Mashitaka haikukubalina na uamzi wa majaji.

Oscar Pistorius aisabahi familia yake kabla ya kupelekwa jela, Oktoba 21 mwaka 2014.
Oscar Pistorius aisabahi familia yake kabla ya kupelekwa jela, Oktoba 21 mwaka 2014. REUTERS/Herman Verwey/Pool

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.