Pata taarifa kuu
ARMENIA-HAKI

Rais wa zamani wa Armenia Sarkisian kujibu mashitaka yanayomkabili

Kesi ya rais wa zamani wa Armenia Serge Sarkisian, anayeshtumiwa ubadhirifu wa mali ya umma, inatarajiwa kuanza Jumanne wiki hii katika mji mkuu wa Armenia, miaka miwili baada ya maandamano ya raia kumtimua madarakani.

Rais wa zamani wa Armenia Serge Sarkissian akiwa bungeni huko Yerevan, Aprili 17, 2018.
Rais wa zamani wa Armenia Serge Sarkissian akiwa bungeni huko Yerevan, Aprili 17, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Serge Sarkisian, 65, alishtakiwa mwezi Desemba na alipigwa marufuku kuondoka kwenye ardhi ya nchi hii ya zamani ya Sovieti. Ikiwa atapatikana na hatia, anakabiliwa na kifungo cha miaka nane.

Waendesha mashtaka wanasema kiongozi huyo wa zamani alihusika katika kutengeneza utaratibu ambapo kampuni ya kibinafsi iliuza mafuta kwa bei ya juu zaidi ikilinganishwa na ile ya sokoni kwa mpango wa msaada wa kilimo wa serikali ya Armenia.

Faida za biashara hiyo haramu, takriban Drams milioni 489 (karibu Euro 946,000 kwa kiwango cha sasa), zilipewa maafisa wakuu na wafanyabiashara, wanasema waendesha mashitaka.

Wakati upande wa mashtaka haujatoa ushahidi wowote mpaka sasa kudhibitisha kwamba Serge Sarkissian alipokea moja kwa moja sehemu ya pesa hizi, mtuhumiwa na chama chake cha siasa wameshutumu kesi hii ambayo wamesema "inalenga kunyamanzisha upinzani" na kuweka hatarini demokrasia.

Serge Sarkissian aliyezaliwa katika mkoa uliojitenga wa Nagorno-Karabakh, ambao uko vitani na Azabajani, alishikilia nyadhifa kadhaa kubwa kabla ya kuwa rais kati ya mwaka 2008 na 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.