Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Marekani kusaidia kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona nchini Korea Kaskazini

media Coronavirus: Idadi ya vifo nchini China imeongezeka hadi 1,423. STR / AFP

Marekani imesema kuwa ina "wasiwasi" kuhusu athari inayowezekana ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona unaofahamika kwa jina la Covid-19 nchini Korea Kaskazini.

Washington iko tayari kuwezesha juhudi za mashirika ya Marekani na ya kimataifa kupambana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo hatari nchini Korea Kaskazini, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imebaini.

"Tunaunga mkono sana na tunapongeza kazi ya mashirika ya kibinadamu ya Marekani na yale ya kimataifa na mashirika ya afya kukabiliana na kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Covid-19 nchini Korea Kaskazini," amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, baada ya Shirika la Msalaba Mwekundu kutoa wito wa Korea Kaskazini kupewa msamaha kwa vikwazo vinavyoikabli kwa kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo nchini humo.

"Marekani iko tayari kuwezesha haraka kutoa idhini ya misaada kutoka kwa mashirika haya," ameongeza Morgan Ortagus katika taarifa.

Mapema Shirikisho la kimataifa la Msalaba Mwekundu lilisema kwamba kuna mahitaji ya haraka ya vifaa vya ulinzi na ugunduzi ili kuzuia uwezekano wa mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 nchini Korea Kaskazini, inayopakana na China Bara ambapo ugonjwa huo ulianzia mwezi Desemba mwaka jana.

Hakuna kesi ya yoyote ya mambukizi ambayo imeripotiwa nchini Korea Kaskazini, ambayo imechukua hatua thabiti kwa watu walio na dalili zinazojulikana za virusi vya ugonjwa wa Covid-19 na imefuta safari za anga na reli na nchi jirani.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana