Pata taarifa kuu
CHINA-AFYA

Corona yaua zaidi ya watu 900

Raia wengi wa China wamesalia nyumbani licha ya muda wa likizo kumalizika leo kwa hofu ya maambukizi ya virusi vya Corona ambavyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 900 na wengine zaidi ya 40,000 kuambukizwa.

Idadi ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa unaofahamika kama Corona inaendelea kuongozeka China na nje ya nchi hiyo.
Idadi ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa unaofahamika kama Corona inaendelea kuongozeka China na nje ya nchi hiyo. STR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Shughuli za kawaida katika miiji mbalimbali, hazijarelewa kama kawaida, huku shule na maduka yakiendelea kufungwa huku kampuni nyingi zikiwaambia wafanyakazi wake, kufanya kazi wakiwa nyumbani.

Serikali nchini humo imetoa wito kwa waajiri kuwarejesha kazini wafanyakazi kwa makundi ili kuepusha idadi kubwa ya watu kuja kazini kwa wakati mmoja, ili kuepusha uwezekano wa maambukizi ya virusi hivyo.

Wakati huo huo, Mawaziri wa afya kutoka mataifa ya bara la Ulaya, watakutana siku ya Alhamisi pamoja na mwakilishi wa Shirika la afya duniani WHO, kujadili maambukizi ya Corona.

Mbali na China, baadhi ya mataifa ya Ulaya, yameripoti maambukizi ya virusi hivi hatari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.