Pata taarifa kuu
CHINA-CORONA-AFYA-MAREKANI

Idadi ya vifo vilivyosababishwa na virusi vya corona yafikia zaidi ya 800 nchini China

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona nchini China imefikia 811 na kwa mara ya kwanza raia wa Marekani na Japan, wamekuwa raia wa kwanza wa kigeni kupoteza maisha wakiwa ugenini.

Abiria akipimwa kutokana na maambukizi ya Corona nchini China
Abiria akipimwa kutokana na maambukizi ya Corona nchini China REUTERS/Aly Song
Matangazo ya kibiashara

Tume ya afya nchini China imetangaza kuongezeka kwa idadi hiyo siku ya Jumapili, idadi ambayo imepita ile ya maambukizi ya SARS, yaliyotokea kati ya mwaka 2002-2003.

Watu wengine 37,198 wameambukizwa kote duniani, wengi wakiwa nchini China.

Hatua ya maafisa wa afya nchini China, kutoa agizo kwa wakuu wa hospitali mbalimbali nchini humo kuteketeza miili ya watu walipoteza maisha kutokana na virusi vya Corona, inaendelea kukosolewa.

Agizo hilo lilitolewa mapema mwezi huu, kama njia mojawapo ya kupambana na maambuzkizi ya virusi hivyo, lakini watalaam wanasema kuwa hatua hii haisaidii.

Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuwa, maambukizi haya sasa ni janga la Kimataifa, na sasa linaomba msaada wa kifedha kusaidia katika mapambano ya virusi hivyo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.