Pata taarifa kuu
CHINA-MAREKANi-USHRIKIANO

Xi Jinping: China ina imani kwamba itatokomeza ugonjwa wa Corona

China ina matumaini ya kuushinda ugonjwa unaofahamika kama Corona, unaotia hofu ulimwengu. Ugonjwa ambao umesababisha vifo vya watu wengi nchini China, huku watu kadhaa wakiripotiwa kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo.

Rais wa China XI Jinping anasema China inaendelea kupambana dhidi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa unaofahamika kama Corona.
Rais wa China XI Jinping anasema China inaendelea kupambana dhidi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa unaofahamika kama Corona. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Katika mazungumzo kwa njia ya simu, rais wa China Xi Jinping amemuhakikishia mwenzake wa Marekani Donald Trump kwamba China itatokomeza ugonjwa hatari unaofahamika kama Corona na kubaini kwamba China ina imani kamili kuhusu uwezo wake wa kuliangamiza janga hilo, vyombo vya habari vya China vimeripoti leo Ijumaa.

Donald Trump ameelezea ameipongeza China kwa kufanya juhudi za kukabiliana na ugonjwa unaofahamika kama Corona, hasa kwa kuchukuwa hatua madhubuti za kuangamiza ugonjwa wa Corona.

Kwa mujibu wa msemaji wa ikulu ya White House, rais wa Marekani Donald Trump ameafikiana na mwenzake wa China kuendelea na uhusiano wa karibu na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Viongozi hao wawili pia wamethibitisha ahadi yao ya kutekeleza hatua zilizotolewa katika makubaliano ya biashara ya "hatua ya 1" yaliyotuiliwa saini mwezi uliopita na Washington na Beijing, amesema Judd Deere.

China ilisema Alhamisi kwamba itapunguza ushuru wa forodha uliowekwa tangu mwaka jana kwa bidhaa zaidi ya 1,700 zilizoingizwa kutoka Marekani.Tangazo hilo limekuja kukiwa na hofu kwamba janga la kiafya linalohusiana na ugonjwa wa Corona lina uzito juu ya ukuaji wa watu ulimwenguni na una athari kwa uhusiano wa kibiashara wa China na Marekani.

Gazeti la Global Times, lenye ukaraibu na Chama cha Kikomunisti nchini China, liliandika Alhamisi kwamba China inapanga kutumia kifungu katika makubaliano ya biashara ya "hatua ya 1" yakiruhusu kuchelewesha utekelezaji wake katika tukio la "majanga ya asili au tukio lingine lisilotarajiwa".

"Kulingana na vyombo vya habari vya China, Xi Jinping amemweleza Donald Trump kwamba China imechukua hatua muhimu kupambana na janga hilo na matunda yameanza kuonekana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.