Pata taarifa kuu
CHINA-AFYA

China: Idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa virusi Corona yaongezeka

Karibu miji kadhaa ya China imewekwa chini ya karantine leo Ijumaa kufuatia mlipuko wa homa inayoambukizwa kutokana na virusi vya Corona.

Maafisa wa polisi wamevaa vifaa maalumu vya kujikinga na  homa inayoambukizwa kutokana na virusi vya Corona, Beijing.
Maafisa wa polisi wamevaa vifaa maalumu vya kujikinga na homa inayoambukizwa kutokana na virusi vya Corona, Beijing. Noel Celis / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo dadi ya vifo imeendelea kuongezeka muda mfupi baada ya Shirika la Afya duniani (WHO) kukataa kutangaza janga hilo kama dharura ya kimataifa.

Watu ishirini na tano wamefariki dunia kwa jumla ya watu 830 walioambukizwa virusi hivy.

"Mwaka huu, Mwaka wetu Mpya unatisha sana," amesema dereva mmoja wa teksi kutoka mji wa Wuhan, jiji lenye wakaazi milioni 11 ambao umewekwa chini ya karantine tangu Alhamisi wiki hii. "Hatuthubutu hata kidogo kuondoka nyumbani kwa sababu ya virusi hivyo, " ameongeza dereva huyo.

Likizo ndefu ya Mwaka Mpya nchini China inaanza leo Ijumaa, katika usiku wa Mwaka wa Panya ambao huanza Januari 25.

Mlipuko wa homa inayoambukizwa kutokana na virusi vya Corona imesababisha kufungwa kwa shughuli za usafiri katika miji miwili ya China.

Baada ya Wuhan wenye wakazi milioni 11 ilipoanzia homa hiyo, imetangazwa kuwa mji mwingine wa Huang-gang wenye wakazi milioni 7.5 umewekwa chini ya karantine kuanzia usiku wa manane jana.

Aina zote za safari zimesimamishwa, na maduka, mikahawa na majumba ya sinema vitalazimishwa kufunga milango.

Hata katika mji mkuu wa China, Beijing, matamasha yote ya kusherehekea mwaka mpya wa kichina yaliyotarajiwa kufanyika mwishoni mwa juma yameahirishwa.

Ripoti ya awali iliyotolewa Alhamisi na tume ya kitaifa ya afya iliripoti vifo vya watu 18 na zaidi ya kesi 600 za maambukizi, huku mkoa wa Hubei, ambao Wuhan ndio mji mkuu, ukiongoza kwa idadi kubwa.

Homa ya virusi vya corona inaambatana na matatizo katika mfumo wa kupumua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.