Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-MAJANGA YA ASILI

Moto wa nyika Australia: Wamarekani watatu wafariki dunia katika ajali ya ndege

Ndege iliyokuwa ikitoa msaada wa kuzima moto kwa kutumia maji kwa minajili ya kukabiliana na moto wa nyika unaoendelea kuathiri maeneo kadhaa ya Australia, imeanguka.

Ndege inayotoa msaada kwa kuzima moto kwa kutumia maji dhidi ya moto wa nyika Januari 10, 2020 huko Penrose, New South Wales, Australia.
Ndege inayotoa msaada kwa kuzima moto kwa kutumia maji dhidi ya moto wa nyika Januari 10, 2020 huko Penrose, New South Wales, Australia. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Wafanyakazi watatuwa ndege hiyo, ambao wote ni raia wa Marekani wamefariki dunia katika ajali hiyo, mamlaka nchini Australia imesema.

Mkuu wa kikosi cha Zima Moto katika maeneo ya vijijini ya New South Wales Shane Fitzsimmons amesema mamlaka nchini Australia imepoteza mawasiliano na ndege hiyo, Lock -ed C-130 Hercules katika eneo la mlima la Snowy Monaro kabla ya 1:30 usiku leo Alhamisi.

Waathiriwa hao watatu ni raia wa Marekani ambao walikuwa ni maafisa wataalam wa kikosi cha Zima Moto waliotumwa na nchi za nje kusaidia kupambana na moto wa nyika unaoendelea kuikumba Australia.

"Tunatoa rambi rambi zetu kwa familia zilizopoteza ndugu zao watatu ambao wamehudumu kwa kipindi cha miaka mingi katika kupambana na moto wa nyika," Shane Fitzsimmons ameongeza.

Idadi ya watu waliofariki tangu kuzuka kwa moto huu wa nyika mwezi Septemba mpaka sasa, ikiwa ni pamoja na wale waliofariki katika ajali hii ya ndege, imefikia 38.

Sababu ya ajali hii bado haijajulikana lakini mapema leo Bwana Fitzsimmons alibaini kwamba upepo mkali "umekuwa ukitatiza" marubani wa ndege hizi kubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.