Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Lebanon yapokea ombi kutoka kwa polisi ya Interpol la kumkamata Carlos Ghosn

media Carlos Ghosn, katika gari akiondoka katika ofisi ya wakili wake baada ya kuachiliwa kwa dhamana, Machi 6, 2019 huko Tokyo. REUTERS/Issei Kato

Polisi ya Interpol imeiomba Lebanon kumkamata mwenyekiti wa zamani wa makampuni ya kutenegeneza magari ya Renault-Nissan aliyekimbilia nchini humo, baada ya kutoroka Japan.

Taarifa hii imethibitishwa na waziri wa sheria wa Lebanon, ambaye amesema serikali ya Lebanon imepokea ombi kutoka kwa polisi ya kimataifa ya Interpol la kumkamata Carlos Ghosn.

"Ofisi ya mwendesha mashtaka (...) imepokea taarifa nyekundu kutoka kwa polisi ya kimataifa ya Interpol kuhusu faili ya Carlos Ghosn," amesema Albert Sarhane, akinukuliwa na shirika la habari la serikali la ANI.

Mwenyekiti wa zamani wa makampuni ya magari Renault-Nissan, ambaye alishtakiwa nchini Japani kwa makosa ya ufisadi, aliwasili nchini Lebanon Jumatatu wiki hii, lakini mpaka sasa makaazi yake hayajulikani yaliko.

Interpol haitoi vibali vya kukamatwa na haiwezi kuanzisha uchunguzi au mashtaka, lakini nchi wanachama na mahakama za kimataifa zinaweza kuomba kuchapishwa kwa "taarifa nyekundu".

Mamlaka nchini Lebanon tayari imetangaza kwamba Ghosn aliingia nchini humo "kihalali" akitumia pasipoti ya Ufaransa na kadi ya kitambulisho cha Lebanon, kwa mujibu wa chanzo kutoka ikulu ya rais.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana