Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-MAJANGA YA ASILI

Watalii hatarini kunaswa kutokana na visa vya moto kuongezeka Australia

Maelfu ya watalii wanaweza kujikuta wamenaswa Kusini Mashariki mwa Australia ambapo nchini kote maafisa wa Zima Moto wanajiandaa kukabiliana na kuongezeka kwa visa vya moto kutokana na wimbi jipya la joto.

Moto wa nyika wanendelea kuyakumba maeneo mbalimbali Australia, hapa ni katika eneo lenye umbali wa kilomita 100 kaskazini mwa Sydney, Disemba 7, 2019.
Moto wa nyika wanendelea kuyakumba maeneo mbalimbali Australia, hapa ni katika eneo lenye umbali wa kilomita 100 kaskazini mwa Sydney, Disemba 7, 2019. SAEED KHAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Moto wa nyika sasa unawaka katika nchi hiyo ya bara la Asia.

Zaidi ya watu 30,000 walitakiwa Jumapili kuodoka katika eneo la kitalii la Mashariki la Gippsland, katika jimbo la Victoria, Kusini-Mashariki mwa nchi, huku viongozi wakihofia kuzuka kwa visa vitatu vya moto mkubwa wa kiwango cha juu kutokana na kuongezeka kwa joto kali, hali ambavyo inaweza kutatiza shughuli mbalimbali kwenye barabara kuu ya mwisho ambayo bado inatumika.

Kamishna wa idara inayokabiliana na majanga katika jimbo hilo, Andrew Crisp, amesema kuwa wakaazi na watu ambao wako katika likizo wanaopatiakana katika eneo hilo wako kwenye hatari ya kukwama.

Bw Crisp amebaini kwamba, "muda wa kuondoka eneo hilo umekwisha" na idara yake haiwezi kuwasaidia chochote.

Maafisa wa Zima Moto wa Australia waendelea kukabiliana na visa vya moto vinavyoendelea kuikumba nchi nzima kama huko Sydney.
Maafisa wa Zima Moto wa Australia waendelea kukabiliana na visa vya moto vinavyoendelea kuikumba nchi nzima kama huko Sydney. PETER PARKS / AFP
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.