Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
Asia

Watu 14 wafariki dunia katika ajali ya ndege Kazakhstan

media Almaty, mji mkuu wa Kazakhstan. Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Almaty imeongeza kwamba ndege hiyo ya shirika la ndege la Bek Air ilipoteza mawasiliano mwendo wa saa moja na dakika 22 , kabla ya kugonga kizuizi kimoja na kuangukia nyumba ya ghorofa mbili. wikipedia

Ndege iliyokuwa ikisafiri na watu 100 imeanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Almaty, nchini Kazakhstan, na kuua watu wasiopungua 14, viongozi katika nchi hiyo ya Asia ya Kati wamesema.

Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Almaty imesema kwamba kulikuwa na abiria 95 na wafanyakazi watano ndani ya ndege hiyo.

'Majeruhi 17 wamelazwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya sana, watu 14 wamekufa papo hapo,' mamlaka ya uwanja wa ndege wa Almaty, jiji kuu la nchi hiyo, imebaini katika ujumbe uliotumwa kupitia ujumbe wa Telegramu.

Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Almaty imeongeza kwamba ndege hiyo ya shirika la ndege la Bek Air ilipoteza mawasiliano mwendo wa saa moja na dakika 22 , kabla ya kugonga kizuizi kimoja na kuangukia nyumba ya ghorofa mbili.

Katika ujumbe wa rambirambi kwenye twitter, Rais Kassym-Jomart Tokayev pia amehakikisha kuwa 'maafisa wawili wataadhibiwa vikali kwa mujibu wa sheria'.

Ajali hiyo ilitokea karibu na Kzyl-tu, mji unaopatikana Kaskazini mashariki mwa uwanja wa ndege wa mji mkuu wa zamani wa Kazakhstan.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana