Pata taarifa kuu
MYANMAR-HAKI

Kiongozi wa Myanmar akana tuhuma dhidi ya nchi yake

Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel na kiongozi wa nchi ya Myanmar, Aung San Suu Kyi, amekana tuhuma dhidi ya nchi yake kuwa imetekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa jamii ya Rohingya ambao wengi ni Waislamu.

Aung San Suu Kyi mbele ya  Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ, Hague ambapo Burma inashtakiwa kwa mauaji ya kimbari, Desemba 11, 2019.
Aung San Suu Kyi mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ, Hague ambapo Burma inashtakiwa kwa mauaji ya kimbari, Desemba 11, 2019. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

Akitoa utetezi wa nchi yake mbele ya majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ, Suu Kyi amekanusha madai aliyosema ni ya uongo yaliyotolewa na nchi ya Gambia kuwa katika operesheni zake za kijeshi mwaka 2017 zililenga waislamu wa Rohingya.

Kiongozi huyo ambaye alitunukiwa tuzo kwa kukosoa jeshi la nchi hiyo, hivi sasa ndio mtetezi wa wanajeshi hao hao wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji ya kiholela, ambapo ameonya mahakama hiyo dhidi ya kujaribu kuchochea mzozo nchini mwake.

Maelfu ya waislamu wa Rohingya, wamekimbia nchi ya Myanmar na kuingia nchi jirani ya Bangladesh wakikwepa mauaji yanayotekelezwa na wanajeshi wa Serikali wanaosema wanawasaka makundi ya waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.