Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Maelfu yaendelea kutikisa jiji la Hong Kong, wanaharakati wataka demokrasia

media Maandamano ya maelfu ya wakaazi wa jiji la Hong Kong Desemba 08 2019 REUTERS/Danish Siddiqui

Maelfu ya waandamanaji wanaopigania demokrasia jijini Hong Kong wameandamana mwishoni mwa wiki iliyopita kuadhimisha miezi 6 tangu kuanza kwa maandamano yao kushinikiza mabadiliko, huku wanaharakati viongozi wakiwaonya wanasiasa wanaouunga mkono utawala wa Beijing.

Maandamano ya hapo jana yanatajwa kuwa makubwa zaidi ukilinganisha na yale yaliyopita, huku waandaaji wakidai kuwa watu zaidi ya laki 8 walijitokeza barabarani kuonesha mshikamano.

Polisi kwenye mji huo ambao mara zote wamekuwa wakiripoti idadi ndogo ya waandamanaji, wamesema watu zaidi ya laki 1 na elfu 83 walishiriki maandamano hayo, ikiwa ni idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodi.

Maandamano haya ambayo yalipata kibali kutoka kwa polisi yamekuja ikiwa ni majuma kadhaa yamepita tangu wanaaharakati wa masuala ya demokrasia wapate ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Wengi wa waandamanaji, walionesha wazi hasira zao dhidi ya kiongozi wa eneo hilo Carrie Lam na utawala wa Beijing ambao wametupilia mbali uwezekano wa kupata suluhu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana