Pata taarifa kuu
CHINA-MAREKANI-USALAMA

Beijing yaonya Marekani kuhusu 'uchokozi' katika Bahari ya China Kusini

China imeitaka Marekani kusitisha luteka za kijeshi katika Bahari ya China Kusini na kuongeza "wasiwasi katika suala la Taiwan, mwakilishi wa China amesema baada ya mazungumzo ya ngazi juu kati ya mawaziri. Kauli hii inaonyesha kuendelea kwa mvutano kati ya Beijing na Washington.

Meli za vikosi vya walinzi kutoka China na Vietnam zikipiga doria kwnye Bahari ya China Kusini.
Meli za vikosi vya walinzi kutoka China na Vietnam zikipiga doria kwnye Bahari ya China Kusini. REUTERS/Nguyen Minh
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Waziri wa Ulinzi wa China Wei Fenghe kwa mwenzake wa Marekani Mark Esper, akinukuliwa na msemaji wa serikali ya China, inakuja wiki mbili baada ya afisa mwandamizi wa Ikulu ya White House kulaani "vitisho" vya China katika lango la Taiwan.

Mark Esper mwenyewe Jumapili alishtumu hadharani Beijing kwa kujaribu kuchukua hatua zaidi na "na vitisho ili kuendeleza malengo yake ya kimkakati" katika ukanda huo.

Wakati wa majadiliano ya faragha katika mkutano wa mawaziri wa ulinzi mjini Bangkok, Wei Fenghe amemsihi Esper "kusitisha luteka za kijeshi kwenye Bahari ya China Kusini na kutochochea au kusababisha mvutano kwenye bahari ya China Kusini, "amesema msemaji wa serikali ya China Wu Qian.

Alipoulizwa kuhusu kile Wei alikuwa akitarajia kutoka Marekani, msemaji huyo amesema: "Marekani iachane na mpango wa kuingilia kati katika Bahari ya China Kusini na kusitisha luteka za kijeshi" katika bahari hiyo.

Taiwan ni moja wapo ya hoja kuu za malumbano kati ya Marekani na China, ambao pia zinvutana katika mzozo wa biashara. Mvutano umeongezeka tangu Wizara ya Ulinzi ya Marekani kuagiza mwezi Julai mwaka huu kuuzwa kwa vifaru vya kijeshi na makombora huko Taipei.

Beijing inadai karibu Bahari zote za China Kusini ni milki yake, madai ambayo Washington inafutilia mbali.

Marekani imeendelea kutuma meli zake za kijeshikatika lango la Taiwan kwa kusema kwamba inaheshimu sheria za kimataifa na inatetea uhuru wa wa kusafiri majini. China inaona kuwa jambo hilo ni kama uchokozi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.