Pata taarifa kuu
HONG KONG-MAANDAMANO-USALAMA

Hong Kong yaendelea kukumbwa na maandamano makubwa

Makabiliano makali yameshuhudiwa kati ya waandamanaji na polisi wa kutuliza ghasia jijini Hong Kong, katika maandamano ambayo yameendelea kwa miezi kadhaa sasa.

Polisi wakijaribu kuwatawanya waandamanaji Tseung Kwan, Hong Kong, China, Novemba 9, 2019.
Polisi wakijaribu kuwatawanya waandamanaji Tseung Kwan, Hong Kong, China, Novemba 9, 2019. . REUTERS/Tyrone Siu
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji hao wengi wakiwa wanafunzi wametumia matofali kupambana na polisi, huku polisi wakitumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwakabili.

Baadhi ya waandamanaji wameonekana wakipambana na polisi na hata kuangushana, katika makabiliano mabaya yaliyotokea katika Chuo Kikuu cha China, katika mji huo wa Hong Kong.

Maafisa wa afya wanasema zaidi ya watu 60 wamejeruhiwa katika makabiliano hayo, huku Umoja wa Ulaya ukitoa wito kwa pande zote mbili kuacha kukabiliana na kuvumiliana.

Marekani pia nayo imesema inasikitishwa na kuendelea kwa maandamano haya ambayo sasa yanatishia hali ya uchumi wa Hong Kong.

Waandamanaji wanasema wataendelea kwa sababu wanapigiania demokrasia ya kisiasa katika eneo hilo, suala ambalo serikali ya China inasema haliwezi kufanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.