Pata taarifa kuu
IRAN-USALAMA

Iran yaanza kurutubisha upya maadini ya urani

Nchi ya Iran imeanza tena urututbishaji wa Urani katika mtambo wake wa chini ya ardhi, Kusini mwa mji mkuu Tehran, ikiwa ni hatua mpya inayoenda kinyume na mkataba wa nyuklia iliyotiliana saini na nchi za magharibi mwaka 2015.

Bendera ya Iran ikiendelea kupepea mbele ya makao makuu ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Vienna, Austria Septemba 9, 2019.
Bendera ya Iran ikiendelea kupepea mbele ya makao makuu ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Vienna, Austria Septemba 9, 2019. REUTERS/Leonhard Foeger
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la nguvu za atomic nchini Iran, wahandisi wake walianza shughuli ya kujaza gesi za urani katika kinu hicho Alhamisi alfajiri.

Mtambo huu ulikuwa ni sehemu ya matakwa ya nchi za Magharibi ambazo ziliitka Iran isitishe shughuli zake kwa kubadilishana na taifa hilo kuondolewa vikwazo.

Uamuzi wa Iran kuanza tena urutubishaji wa urani katika kinu chake cha Fordow, umekosolewa vikali na mataifa mengine yaliyosalia kwenye mkataba huo ambao Marekani ilijitoa na kurejesha vikwazo dhidi ya utawala wa Tehran.

Tayari Marekani imeionya Iran dhidi ya kuendelea na mpango wake wa kufufua vinu zaidi ambavyo ilivizima wakati ikikubali kuwa sehemu ya nchi hiyo kuondolewa vikwazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.