Pata taarifa kuu
UFARANSA-CHINA-USHIRIKIANO-UCHUMI

Emmanuel Macron azuru China, mikataba kadhaa kutiwa saini

Emmanuel Macron anaendelea na ziara ya serikali nchini China. Atafanya ziara ya siku tatu Shanghai na Beijing. Lengo la ziara hiyo ya rais wa Ufaransa ni kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Emmanuel Macron arejea China mwaka na nusu baada ya ziara yake ya kwanza ya serikali (picha ya kumbukumbu).
Emmanuel Macron arejea China mwaka na nusu baada ya ziara yake ya kwanza ya serikali (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Thomas Peter
Matangazo ya kibiashara

Mikataba kadhaa inatarajiwa kutiwa saini wakati wa ziara hiyo, haswa katika sekta ya kilimo na nishati.

Ikiwa suala la mgogoro mkubwa wa kimataifa na suala la tabia nchi litakuwa kwenye ajenda ya mazungumzo ya wawili hao, swala la kibiashara, litapewa kipaumbele katika ziara hii kama mwaka jana, wakati ambapo rais wa Ufaransa pia anatazamiwa kuzindua ofisi mpya ya Kituo George Pompidou jijini Shanghai.

Ufaransa inatarajia kuishawishi China kuimarisha uhusiano wake na Ufaransa katika nyanja mbalimbali. Rais Macron atataka "kueza tena sawa uhusiano wa nchi mbili"; kwani hata kama mikataba zaidi ya arobaini inatarajiwa kutiwa saini wakati wa ziara hii, nakisi ya biashara ya Ufaransa na China inasalia kuwa mbaya, hadi kiwango cha euro bilioni 29.

Kwa hivyo suala hili pia litakuwa kwenye ajenda ya mazungumzo kati ya Emmanuel Macron na mwenyeji wake Xi Jinping, kuanzia Jumatatu hii jioni wakati wa chakula cha kwanza cha jioni, na Jumanne usiku wakati wa chakula cha jioni kabla ya uzinduzi wa maonyesho ya bidhaa kutoka Shanghai, ambapo Ufaransa ambayo inatafuta kushiriki kwenye soko la China, ni mgeni wa heshima.

Rais wa Ufaranda Emmanuel Macron anaambatana na viongozi hamsini wa makampuni mbalimbali, kama Airbus, Oreal, Sanof, lakini pia SME, Devialet na Deezer.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.