Pata taarifa kuu
IRAQ-IRAN-USALAMA

Khamenei ashutumu maadui kwa kujaribu kuchochea mzozo kati ya Tehran na Baghdad

Kiongozi Mkuu wa Irani Ali Khamenei ameshtumu "maadui" kwa kujaribu "kuchochea mzozo" kati ya Irani na Iraq, ambayo inaendelea kukumbwa kwa karibu wiki moja na maandamano ambayo yamesababisha watu zaidi ya 100 kupoteza maisha.

Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, Tehran, Julai 16, 2019.
Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, Tehran, Julai 16, 2019. Official Khamenei website/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Iran na Iraq ni mataifa mawili ambayo yameunganishwa kwa mambo mengi. Maadui watafuta kupandikiza mzozo lakini wameshindwa na njama zao hazitafikia popote pale", Khamenei ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu "maadui" hao ambao hakuwataja.

Kwa mujibu wa shirika la habari serikali la Irna, ujumbe huo wa Twitter umechapishwa ili kukabiliana na maandamano nchini Iraq, haswa huko Baghdad na kusini mwa nchi hiyo, eneo lenye Washia wengi tangu Oktoba 1. Waaandamanaji wanataka serikali kujiuzulu wakiishtumu ufisadi na mageuzi ya kiuchumi bila kuzingatia maslahi ya wananchi.

Mamlaka nchini Iraq imewashutumu "matapeli" nakuwalenga waandamanaji na polisi. Kulingana na vyanzo vya matibabu na usalama, miongoni mwa watu zaidi ya mia moja waliouawa, wanane ni askari. Zaidi ya watu 6,000 wamejeruhiwa katika maandamano hayo.

Maandamano hayo yanakuja wakati maelfu ya waandamanaji wa Irani wakianza Hija ya kila mwaka ya Kishia kwenye kaburi la Imam Hussein jijini Kerbala, kilomita 110 kusini mwa Baghdad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.