Pata taarifa kuu
HONG KONG-MAANDAMANO-USALAMA

Wanafunzi wapanga kususia shule Hong Kong

Hong Kong inaendelea kukumbwa na maandamano. Baada ya vurugu mwishoni mwa wiki hii iliyopoita kati ya polisi na waandamanaji, maandamano mapya yanatarajia kufanyika leo, wanafunzi wakiwa katika mstari wa mbele.

Waandamanaji wanabebelea mabango ya yenye maneno ya kuunga mkono demokrasia. Hong Kong, Septemba 2, 2019.
Waandamanaji wanabebelea mabango ya yenye maneno ya kuunga mkono demokrasia. Hong Kong, Septemba 2, 2019. REUTERS/Kai Pfaffenbach
Matangazo ya kibiashara

Wanafunzi wa shule za sekondari katika jiji la Hong Kong wanatarajia kugoma shule kama ishara ya kuunga mkono mwendelezo wa maandamano ya kuipinga serikali.

Wanafunzi wanapanga kuanza mgomo leo alasiri na kukusaniyka kwenye uwanja uliopo kati kati ya mji wa Hong Kong. Pamoja na madai mengine wanafunzi hao wanataka kufutwa kwa mashtaka yanayowakabili waandamanaji waliokamatwa.

Maandamano haya yanatarajia kudumu wiki mbili. Mwaka wa shule Hong Kong umeanza leo Jumatatu.

Waandamanaji wanataka mageuzi ya mfumo wa uchaguzi na uchunguzi huru ufanywe juu ya tabia ya vitendo vya polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.