Pata taarifa kuu
HONG KONG-MAZUNGUMZO-USALAMA

Mgogoro Hong Kong: Carrie Lam ataoa wito kwa waandamanaji kushirikia mazungumzo

Siku mbili baada ya maelfu ya waandamanaji kumiminika katika mitaa ya Hong Kong siku ya Jumapili, na baada ya majuma 11 ya maandamano yaliyogubikwa na machafuko, Rais wa Serikali ya Hong Kong amewataka waaandamanaji kushiriki mazungumzo yanayotarajia kufanyika.

Rais wa serikali ya Hong Kong, Carrie Lam, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Agosti 20, 2019.
Rais wa serikali ya Hong Kong, Carrie Lam, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Agosti 20, 2019. REUTERS/Ann Wang
Matangazo ya kibiashara

Carrie Lam amesema yuko tayari kuketi kwenye meza ya mazungumo na waandamanaji.

Carrie Lam ambaye alipatwa na hasira baada ya wakaazi wa eneo hilo kuingia mitaani mitaani, kutokana na sheria yake inayoagiza washtumiwa kutumwa kwenye mahakama ya China bara, amejeleza katika mkutano na waandishi wa habari leo Jumanne.

Hakukuwa na taarifa ya kutatanisha kuhusu muswada huo. Carrie Lam amekataa kujikubalisha kufuta muswada huo. Kwa upande mwingine, amesema kwamba utawala wake ulikuwa unafanya kazi ili kuanzisha mazungumzo kwa lengo la kumaliza mzozo huo.

"Pamoja na timu yangu, tumejitolea kusikiliza kile watu wanachotaka kusema," amesema Carrie Lam, akibaini kwamba ataungana na makundi ambayo yanataka mazungumzo, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.Akizungumzia maandamano makubwa ya Jumapili, amesem aana imani kwamba hali hiyo inamaanisha kurudi kwa amani, baada ya majuma ya machafuko na vurugu kati ya polisi na waandamanaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.