Pata taarifa kuu
HONG KONG-MAANDAMANO-USALAMA

Waandamanaji waapa kuendelea na maandamano Hong Kong

Jiji la Hong Kong linakabiliwa kukumbwa na maandamano mengine makubwa zaidi mwishoni mwa juma. Waandamanaji wanaounga mkono demokrasia katika mji wa Hong Kong wameapa kuminika kwa wingi katika mitaa mbalimbali ya mji huo.

Mazoezi ya majeshi ya China, Shenzhen Agosti 15, 2019.
Mazoezi ya majeshi ya China, Shenzhen Agosti 15, 2019. REUTERS/Thomas Peter
Matangazo ya kibiashara

Polisi imepiga marufuku mikusanyiko katika maeneo mbalimbali, isipokuwa katika hifadhi ya wanyama ya Victoria Park. Haitoshi, "kwa sasa", kuwazuia waandamanaji. Maandamano makubwa yanatarajiwa kufanyika licha ya vitisho kutoka mamlaka nchini Cchina.

Katika siku za hivi karibuni, vyombo vya habari vya serikali vilirusha picha za kuvutia za malori ya jeshi, mizinga, polisi wakifanya gwaride katika uwanja wa mpira wa Shenzhen kilomita chache kutoka Hong Kong.

China imeonya dhidi ya mataifa ya nje kuuingilia mgogoro huo, wakati wanajeshi wa China Bara wakionekana kufanya mazoezi ya kijeshi mpakani mwa Hong Kong. Serikali za Magharibi ikiwemo Marekani zimetoa wito wa uvumilivu kutokana na matukio ya vurugu wakati wa maandamano katika uwanja wa ndege wiki hii ,yaliyosababisha safari takriban 1,000 za ndege kufutwa.

Katika maandamano hayo waandamanji waliwashambulia watu wawili walioshukiwa kuwa vibaraka vya serikali. Hali katika uwanja wa ndege wa Hong Kong uliyo na shughuli nyingi imeanza kurejea kama kawaida lakini chini ya ulinzi mkali baada ya waandamanaji kujazana huko siku ya Jumatatu na Jumanne usiku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.