Pata taarifa kuu
URUSI-AJALI

Ndege ya Urusi yatua kwa dharura katika shamba la mahindi, 23 wajeruhiwa

Urusi imekaribisha hatua ya kishuja na ya kushangaza ya marubani wa ndege aina ya Airbus A321, ambao walilazimika kutua kwa dharura leo Alhamisi katika shamba la mahindi. Ndege hiyo ambayo iligonga kundi la ndege angani, ilikuwa imeabiri watu 233.

Airbus 321, ndege ya shirika la ndege la Urusi laUral Airlines ililazimika kutua kwa dharura katika shamba la mahindi, karibu na Uwanja wa Ndege wa Zhukovsky, Agosti 15, 2019.
Airbus 321, ndege ya shirika la ndege la Urusi laUral Airlines ililazimika kutua kwa dharura katika shamba la mahindi, karibu na Uwanja wa Ndege wa Zhukovsky, Agosti 15, 2019. REUTERS/Stringer.
Matangazo ya kibiashara

Mapema asubuhi, ndege ya shirika la ndege la Urusi la Ural Airlines iliondoka kutoka uwanja wa ndege wa Zhukovsky, katika kitongoji cha mji mkuu Moscow, kuelekea Simferopol, mji mkuu wa rasi ya Ukraine ya Crimea uliounganishwa na Urisi mnamo mwaka 2014.

Lakini wakati wa kuondoka, ndege hiyo iliokuwa imeabiri watu 226 na wafanyakazi 7 "iligonga kundi la ndege", ambapo ndege kadhaa zilijikuta katika injini za chombo hicho cha Airbus na kusababisha "usumbufu mkubwa katika safari yake, "kwa mujibu wa mamlaka ya safari za anaga nchini Urusi, Rosaviatsia.

Wafanyikazi wa ndege hiyo waliamua kutua kwa dharura "katika chamba wa mahindi (...) linalopatikana zaidi ya kilomita moja kutoka eneo la ndege kupaa angani," mamlaka ya safari za anga nchini Urusi imebaini, huku ikibaini kwamba hakuna hasara kubwa iliyotokea upande wa abiria, ispokuwa abiria 23 pekee ambao wamejeruhiwa.

Watu 23 wakiwemo watoto 9 wamejeruhiwa katika tukio hilo la kushangaza, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Urusi. Ishirini na mbili kati yao walipewa huduma ya matibabu kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani, wakati mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 69 alilazwa hospitalini, wizara hiyo imesema katika taarifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.