Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Kumi na nne wauawa katika mapigano kati ya jeshi na waasi masharikimwa Burma

media Wapiganaji wa Jeshi la Kitaifa la Ukombozi Taaung, moja ya makundi kubwa vya waasi Kaskazini mashariki mwa Burma, Januari 16, 2014 © AFP

Karibu watu 14 wameuawa leo Alhamisi mashariki mwa Burma katika mapigano kati ya jeshi na makundi ya waasi. Mapigano hayo yametokea kwa mara ya kwanza katika shule ya kijeshi.

Mashambuliz matano yalitekelezwa na makundi ya waasi wa kikabila Alhamisi asubuhi katika mji wa Pyin Oo Lwin, mji wa kitalii karibu na Mandalay ambapo kunapatikana kambi kadhaa za jeshi. Shule ya kijeshi imelengwa hasa na roketi.

Jeshi limejibu mashambulizi hayo kwa kuzindua operesheni dhidi ya makundi hayo.

Mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP ameshuhudia miili ya askari saba na polisi wanne katika kituo cha polisi kilichoshambuliwa.

Katika eneo jingine, watu wengine watatu, askari wawili na raia mmoja, wameuawa na mapigano "yanaendelea", amesema msemaji wa jeshi Brigadia Zaw Min Tun.

Jeshi la Kitaifa la Ukombozi la Taaung (TNLA), moja ya makundi makubwa ya waasi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, limedai kuhusika na mashambulizi hayo kwa kulipiza kisasi kwa operesheni za jeshi."

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana