Pata taarifa kuu
BURMA-USALAMA

Kumi na nne wauawa katika mapigano kati ya jeshi na waasi mashariki mwa Burma

Karibu watu 14 wameuawa leo Alhamisi mashariki mwa Burma katika mapigano kati ya jeshi na makundi ya waasi. Mapigano hayo yametokea kwa mara ya kwanza katika shule ya kijeshi.

Wapiganaji wa Jeshi la Kitaifa la Ukombozi Taaung, moja ya makundi kubwa vya waasi Kaskazini mashariki mwa Burma, Januari 16, 2014
Wapiganaji wa Jeshi la Kitaifa la Ukombozi Taaung, moja ya makundi kubwa vya waasi Kaskazini mashariki mwa Burma, Januari 16, 2014 © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashambuliz matano yalitekelezwa na makundi ya waasi wa kikabila Alhamisi asubuhi katika mji wa Pyin Oo Lwin, mji wa kitalii karibu na Mandalay ambapo kunapatikana kambi kadhaa za jeshi. Shule ya kijeshi imelengwa hasa na roketi.

Jeshi limejibu mashambulizi hayo kwa kuzindua operesheni dhidi ya makundi hayo.

Mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP ameshuhudia miili ya askari saba na polisi wanne katika kituo cha polisi kilichoshambuliwa.

Katika eneo jingine, watu wengine watatu, askari wawili na raia mmoja, wameuawa na mapigano "yanaendelea", amesema msemaji wa jeshi Brigadia Zaw Min Tun.

Jeshi la Kitaifa la Ukombozi la Taaung (TNLA), moja ya makundi makubwa ya waasi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, limedai kuhusika na mashambulizi hayo kwa kulipiza kisasi kwa operesheni za jeshi."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.