Kulingana na taarifa ya Wizara ya afya nchini humo afisa mmoja aliuwawa kwa kupigwa risasi na watu wengine 36 walijeruhiwa.
Awali shirika la habari la Interfax lilimnukuu Waziri wa usalama wa ndani nchini humo akisema maafisa wa usalama wanaondoka katika eneo hilo kutokana na utekaji nyara unaofanywa na wafuasi wa Atambayev.
Almazbek Atambayev alishtakiwa mwishoni mwa mwezi Juni kwa ufisadi. Alivuliwa kinga baada ya kutuhumiwa kashfa hiyo.
Almazbek Atambayev alifutilia mbali tuhuma hizo dhidi yake na hadi sasa amekataa kufika mahakamani.