Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Pakistan yaashutumu India kwa kutumia itikadi kali za kibaguzi

media Wafuasi wa chama cha siasa cha kidini Jamaat-e-Islami (JI) wakiimba nyimbo zinazopinga serikali ya India wakati wa maandamano Islamabad Agosti 6, 2019, siku moja baada ya India kutupilia mbali hoja ya kujitawala kwa Jimbo la Kashmir. AAMIR QURESHI / AFP

Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan ameapa kupinga uamuzi wa serikali ya India kuondoa uhalali wa jimbo linalojitegemea la Kashmiri, vita ambavyo amesema atavipeleka katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Khan amesema hatua hiyo ya India haikubaliki na inakwenda kinyume cha sheria za kibinadamu, na kuelekeza kuwa kinachoendelea ni mauaji ya kikabila.

Shughuli zimekwama katika jimbo hilo, baada ya uamuzi huo tata wa India.

Kashmir ni jimbo ambalo linawaniwa na nchi ya India na Pakistan, na ni eneo la mzozo kati ya nchi hizo mbili.

Hali hii imeendelea kusababisha utovu wa usalama katika jimbo hilo kwa kuwepo kwa kundi la wapiganaji ambalo kwa zaidi ya miaka 30, limewauwa maelfu ya watu.

Mbali na Pakistan, nchi jirani ya China pia imelaani hatua hiyo na kusema haikubaliki.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana