Pata taarifa kuu
HONG KONG-USALAMA

Hong Kong yaendelea kukumbwa na vurugu

Mji wa Hong Kong umeshuhudia vurugu kubwa hapo jana baada ya kutokea makabiliano kati ya waandamanaji na polisi ambao walitumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kujaribu kuwatawanya.

Maandamano makubwa Hong Kong, polisi yatumia gesi ya machozi ili kusambaratisha waandamanaji, Hong Kong, Julai 21, 2019.
Maandamano makubwa Hong Kong, polisi yatumia gesi ya machozi ili kusambaratisha waandamanaji, Hong Kong, Julai 21, 2019. ANTHONY WALLACE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Moshi wa mabomu ya kutoa machozi ulienea kwa sehemu kubwa katika jiji la Hong Kong ambapo polisi walikuwa wakikabiliana na mamia ya waandamanaji waliokuwa wamevalia nguo zilizoficha nyuso zao.

Awali yalianza kama maandamano ya amani kabla ya kugeuka kuwa ya vurugu pale waandamanaji walipoanza kurusha mayai kulenga majengo ya ofisi za Serikali na kuchora kuta kueleza kuchukizwa na namna utawala wa Beijing unaingilia mamlaka ya mji huo.

Maandamano ya majuma kadhaa yaliyopita yalikuwa ya kupinga sheria tata ya kubadilishana watuhumiwa na Beijing, lakini tangu wakati huo kumeibuka maandamano mengine ya kushinikiza mabadiliko ya kidemokrasia na uhuru wa watu kujieleza.

Haya ni maandamano makubwa zaidi kwa serikali ya China kushuhudia tangu eneo la Beijing lirejeshwe kama sehemu ya China mwaka 1997.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.