Pata taarifa kuu
UINGEREZA-IRAN-USHIRIKIANO-USALAMA

London yaishtumu Tehran kutaka kuzuia njia meli yake ya mafuta Hormuz

Ghuba ya Kiajemi ni eneo linalo zozaniwa kati ya Iran na Uingereza. Hali hii imeripotiwa kwanza na televisheni ya Marekani ya CNN, na kuthibitishwa Alhamisi, Julai 11 na London.

Meli ya mafuta ya Uingereza, Heritage, Machi 2019.
Meli ya mafuta ya Uingereza, Heritage, Machi 2019. REUTERS/Cengiz Tokgoz
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo jeshi la Iran limekana kuizuwia njia meli ya mafuta ya Uingereza.

Meli tatu za kijeshi za Irani zimejaribu kuzuia njia meli ya mafuta ya Uingereza katika mlango bahari wa Hormuz, kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Uingereza.

Jeshi la wanamaji la Uingereza lililazimika kuingilia kati kwa kutoa msaada kwa meli hiyo ya kibiashara ili kuzuia mashambiulizi ya Iran.

Tukio hili jipya linakuja wakati mgogoro kuhusu nyuklia ya Iran ukiendelea.

Wakati huo huo Mkuu wa majeshi ya Ufaransa Francois Lecointre amesema leo baada ya Uingereza kuishutumu Iran kuzisumbua meli za mafuta za nchi hiyo kuwa, hali ya wasi wasi katika eneo la Ghuba haielekei kufikia kiwango cha kutoweza kudhibitiwa.

Kwa mujibu wa Uingereza, mkasa huo ulitokea Jumatano wiki hii kwenye mlango wa bahari wa Hormuz, muda mchache baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kurejelea vitisho vyake vya kuongeza vikwazo vikali dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.