Pata taarifa kuu
IRANI-MAREKANI-VIKWAZO-USHIRIKINAO

Vikwazo vipya vya Marekani: Tehran yapandwa na hasira na kujibu

Tehran inasema imechukua hatua dhidi ya vikwazo vipya vya Marekani. Rais wa Marekani Donald Trump ameamua kuweka vikwazo vipya dhidi ya kiongozi mkuu wa wa dini nchini Iran na makamanda kadhaa wa ikosi cha Ulinzi wa Mapinduzi, kikosi chenye ushawishi mkubwa nchini Iran.

Ayatollah Ali Khamenei alengwa na vikwazo vipya vilivyowekwa na Washington (picha ya kumbukumbu).
Ayatollah Ali Khamenei alengwa na vikwazo vipya vilivyowekwa na Washington (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Caren Firouz/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivyo vinakuja baada ya shambulizi dhidi ya ndege isiyo kuwa na rubani ya Marekani.

Katika ukurasa wake wa Twitter kwa lugha ya Kiajemi, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa "vikwazo dhidi ya Kiongozi Mkuu dini na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, inamaanisha kufungwa moja kwa moja kwa ushirikiano wa kidiplomasia na serikali ya sasa ya Marekani."

Abbas Moussavi ameshtumu serikali ya Donald Trump kwamba imevunja jitihada zote za kimataifa za kutunza amani na usalama duniani.

Kwa kumuwekea vikwazo kiongozi mkuu, Ayatollah Ali Khamenei, Marekani imevuka mstari mwekundu kwa jinsi Tehran inavyomuheshimu.

Kiongozi wa Irani alisema wiki mbili zilizopita wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Japan nchini humo, ambaye alikuja Tehran juu ya ujumbe wa usuluhishi, kuwa atakataa mazungumzo yoyote na rais wa sasa wa Marekani.

Itakumbukwa kwamba nchi hizo mbili zilivunja uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1980.

Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito wa kufanyika majadiliano na kutafuta suluhu itakayomaliza mzozo kwenye eneo la Ghuba, wito ambao hata hivyo Iran imekataa kuwa na mazungumzo na Marekani baada ya rais Donald Trump kutangaza vikwazo zaidi.

Katika azimio lililowasilishwa na Kuwait, nchi wanachama ziliunga mkono wito wa kufanyika mazungumzo na kulaani mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya meli za mafuta.

Iran yenyewe inasisitiza kuwa vikwazo vilivyotangazwa na Marekani havitaitikisa na badala yake vitaifanya nchi hiyo kuwa imara zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.