Pata taarifa kuu
UN-IS-JAMII-USALAMA

Umoja wa Mataifa wataka familia za wanajihadi kurejeshwa makwao

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa amependekeza kurejeshwa kwenye nchi zao, maelfu ya ndugu na wanafamilia wa watuhumiwa wa kundi la Islamic State.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Michelle Bachelet. (Picha ya kumbukumbu).
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Michelle Bachelet. (Picha ya kumbukumbu). REUTERS/Lucas Jackson
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika kongamano la mwaka la tume ya haki za binadamu mjini Geneva, Michelle Bachelet amesema hasa watoto, wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki zao.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto Unicef linakadiria kuwa, kuna watoto elfu 29 wa wapiganaji wa kigeni wa islamic State nchini Syria ambao elfu 20 wanatokea Iraq.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema kwa sasa jumla ya wapiganaji elfu 55 wa Islamic State pamoja na familia zao wanazuiliwa kwenye nchi za Syria na Iraq baada ya kundi hilo kumalizwa, huku wengi wakitokea kwenye mataifa hayo mawili licha ya kuwa wapo wanaotoka kwenye mataifa zaidi ya 50 duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.