Pata taarifa kuu
HONG KONG-CHINA-SIASA-MAANDAMANO

Kiongozi wa Hong Kong aomba radhi kuhusu mswada tata

Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam, ameomba radhi kwa namna serikali yake inavyoshughulikia mswada tata unaoruhusu washtakiwa wa makosa mbalimbali kufikishwa katika Mahakama nchini China.

Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam
Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam 路透社
Matangazo ya kibiashara

Licha ya kuomba radhi, Lam ambaye anaungwa mkono na serikali ya China, hajasema iwapo mswada huo unafutwa.

“Binafsi nawajibikia mswada huu ambao umezua sintofahamu katika jamii,” alisema.

“Kutokana na hili, nawaomba radhi watu wote wa Hong Kong,” aliongeza.

Mswada huo umezua maandamano makubwa, huku waandamanaji wakiendelea kumshikiniza Bi. Lam ajiuzulu wadhifa huo.

Wanaharakati na wanasiasa wa upinzani, wanadai kuwa mswada huo unawalenga kwa sababu ya tofauti zao za kisiasa na serikali ya Beijing.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.