Pata taarifa kuu
CHINA

Maelfu waandamana Hong Kong kupinga sheria tata

Kiongozi wa jiji la Hong Kong, Carrie Lam amesema hana mpango wa kuondoa sheria tata itakayoruhusu kusafirishwa kwa watuhumiwa kwenye bara, kauli anayotoa siku moja tu baada ya watu zaidi ya milioni moja kuandamana kupinga sheria hiyo.

Malefu ya waandamanaji kwenye mji wa Hong Kong wakiwa na mabango kukashifu serikali ya mji huo.
Malefu ya waandamanaji kwenye mji wa Hong Kong wakiwa na mabango kukashifu serikali ya mji huo. REUTERS/Thomas Peter
Matangazo ya kibiashara

Lam akiongea na wanahabari amesema sheria hiyo ni muhimu na itasaidia kulinda haki na kuhakikisha Hong Kong inatimiza takwa la sheria za kimataifa kuhusu wahalifu.

Licha ya ukosolewaji mkubwa kutoka kwa wabunge na watetezi wa haki za binadamu pamoja na maandamano kupinga sheria hiyo, Lam ameonekana kuweka ngumu kubadili msimamo wake.

Tangu wakati alipopendekeza kupitishwa kwa sheria hiyo, wabunge na raia walionesha wazi kuipinga sheria hiyo wanayosema inakiuka haki za binadamu wakati huu wakiutuhumu utawala wa Bara kwa kujaribu kutumia nguvu dhidi yao.

Polisi wa kutuliza ghasia walizingira ofisi za bunge baada ya kushuhudia maandamano yakigeuka vurugu ambapo mamia ya waandamanaji walikabiliana na vyombo vya usalama vilivyotumia maji ya pilipili kukabiliana na waandamanaji.

Maandamano haya yalilenga kuongeza shinikizo zaidi kwa utawala wa Lam ambao unaunga mkono Serikali ya Beijing.

Wanasiasa wakongwe kwenye eneo hilo wamemtaka Lam ajiuzulu nafasi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.