Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 13/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Mfalme wa Japani akabidhi madaraka kwa mwanae wa kiume

media Kwa upande wa kushoto, Mfalme Showa kwa jina maarufu Hirohito (1901-1989). Kwa upande wa kulia, mwanae Akihito, aliyezaliwa mwaka 1933 na ambaye wananchi wa Japani watamwita Heisei baada ya kustaafu. AFP PHOTO/FILES

Kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka 200, Mfalme wa Japani anaachia madaraka hivi leo, na kumkabidhi mwanae wa kiume Prince Naruhito.

Mfalme Akihito mwenye umri wa miaka 85, anastaafu na kukabidhi madaraka kwa mtoto wake wa kiume, Mwanamfalme Naruhito, mwenye umri wa miaka 59, katika makabidhiano ambayo yatachukua dakika 10 hivi.

Hatua hii inaanzisha historia mpya, iloyopewa jina la Reiwa, na wananchi wa Japan watakuwa na mapumziko ya siku 10 kumkaribisha kiongozi mpya.

Mnamo mwezi Juni 2017 Bunge la Japan lilipitisha muswada unaotoa ruhusa kwa Mflame Akihito kujivua madaraka yake na kuwa mfalme wa kwanza kufanya hivyo katika kipindi cha miaka 200.

Mfalme huyo wa Japan mwenye miaka 8 alisema mwaka 2016, umri wake na afya yake unamfanya kushindwa kutimiza majukumu yake vizuri.

Mfalme Akihito na Malkia Michiko wamesimamia kipindi cha mabadiliko makubwa Japan na kuwa karibu zaidi na raia. Maelfu ya watu hufika kila mwaka mpya makao makuu ya kifalme kuwatakia heri.

Akihito ndiye Mfalme wa 125 katika familia ya kifalme ambayo inaaminika kutawala tangu karne ya tano, jambo linaloifanya kuwa familia ya kifalme ya kale zaidi duniani.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana