Pata taarifa kuu
SRI LANKA-USALAMA-UCHUNGUZI

Ulinzi waendelea kuimarishwa Sri Lanka

Waumini wa madhehebu ya Kikristo nchini Sri Lanka, siku ya Jumapili wamelazimika kufanya misa wakiwa majumbani mwao baada ya Serikali kuzuia kufunguliwa kwa makanisa.

waombolezaji walifanya ibada kuwakumbuka ndugu na marafiki zao waliopoteza maisha katika shambulio la juma lililopita ambapo watu 253 waliuawa.
waombolezaji walifanya ibada kuwakumbuka ndugu na marafiki zao waliopoteza maisha katika shambulio la juma lililopita ambapo watu 253 waliuawa. REUTERS/Thomas Peter
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa Serikali umetokana na hofu ya kutekelezwa kwa mashambulizi zaidi, huku viongozi wa makanisa wakikashifu shambulio la juma lililopita, wakisema lilikuwa ni udhalilishaji na halina utu.

Serikali ya Sri Lanka imetetea uamuzi wake ikisema imelazimika kuchukua tahadhari kutokana na kuwepo kwa wasiwasi wa kutekelezwa kwa mashambulizi mengine ya kigaidi kulenga makanisa.

Ulinzi uliimarishwa kwenye makanisa mengi ambapo waombolezaji walifanya ibada kuwakumbuka ndugu na marafiki zao waliopoteza maisha katika shambulio la juma lililopita ambapo watu 253 waliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.