Pata taarifa kuu
JAPAN-GHOSN-UCHUMI-HAKI

Bosi mstaafu wa Renault-Mitsubishi-Nissan aachiwa kwa dhamana, Japan

Aliyekuwa Mkurugenzi wa kampuni za kutengeza magari Renault-Mitsubishi-Nissan,Carlos Ghosn, amepewa dhamana ya Dola Milioni 4.5 na Mahakama jijiji Tokyo.

Carlos Ghosn (kushoto) na mkewe Carole wakiondoka katika ofisi ya mwanasheria Junichiro Hironaka, 3 Aprili 2019, Tokyo
Carlos Ghosn (kushoto) na mkewe Carole wakiondoka katika ofisi ya mwanasheria Junichiro Hironaka, 3 Aprili 2019, Tokyo © AFP
Matangazo ya kibiashara

Ghosn alikamatwa mwaka uliopita, baada ya madai ya matumizi mabaya ya fedha na madaraka alipokuwa anaongoza kampuni hiyo.

Hata hivyo, viongozi wa mashtaka wamesema watakataa rufaa, uamuzi wa Mahakama kumwachilia Ghosn kwa dhamana.

Awali Ghosn aliachiwa kwa dhamana yenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 8.9 baada ya kushikiliwa kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu.

Kiongozi huyo wa zamani wa kampuni ya Nissan anatuhumiwa kutumia vibaya madaraka yake sambamba na matumizi mabaya ya fedha pamoja na kukosa uaminifu wakati akiongoza Kampuni hivyo na kusababisha kufunguliwa mashtaka.

Awali ombi lake la kupatiwa dhamana lilitupwa mbali na Mahakama ya Tokyo hatua iliyofanya Jumuiya ya Kimataifa kukosoa uamuzi huo na kuongeza shinikizo kwa nchi ya Japan na hatimaye Mahakama imebadili uamuzi wake.

Waendesha mashitaka jijini Tokyo walimkamata kwa mara ya nne aliyekuwa mwenyekiti wa Nissan Motor Carlos Ghosn kwa kushukiwa kukiuka uaminifu.

Waendesha mashitaka wamesema Ghosn aliagiza sehemu ya fedha za Nissan zipelekwe kwa kampuni mshirika ya Oman inayoendeshwa na mtu anayefahamiana naye. Malipo hayo yalifanyika kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka jana. Anashukiwa kuisababishia Nissan hasara ya takribani dola milioni 5 kufuatia muhamala huo wa kifedha.

Vyanzo vyenye taarifa za kina vilisema baadhi ya malipo kwa kampuni mshirika ya Oman yalifanyika kupitia kampuni ghushi ya nchini Lebanon kupitia akaunti ya kampuni inayoendeshwa na afisa mtendaji, raia wa India.

Fedha hizo zinaaminika kutumika kununulia boti ya kifahari ya Ghosn na pia huenda zilipelekwa kwenye kampuni ya uwekezaji iliyopo nchini Marekani inayomilikiwa na mtoto wa kiume wa Ghosn.

Ghosn aliachiwa mnamo Machi 6 baada ya kushikiliwa kwa siku 108.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.