Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-URUSI-USHIRIKIANO

Mkutano wa kwanza kati ya Kim na Putin kufanyika Alhamisi Vladivostok

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un atakutana na rais wa Urusi Vladimir Putin Alhamisi wiki hii katika mji wa Vladivostok, kwenye bandari ya Mashariki mwa Urusi katika bahari ya Pasifiki, mshauri wa Kremlin amesema.

Wawili hao watajadili jitihada zinazoendelea za kisiasa na kidiplomasia ili kutatua suala la nyuklia kwenye rasi ya Korea, Yuri Ushakov amesema.
Wawili hao watajadili jitihada zinazoendelea za kisiasa na kidiplomasia ili kutatua suala la nyuklia kwenye rasi ya Korea, Yuri Ushakov amesema. REUTERS/Jorge Silva et Maxim Shipenkov
Matangazo ya kibiashara

Huu utakuwa mkutano wa kwanza kati ya viongozi hao wawili. Wawili hao watajadili jitihada zinazoendelea za kisiasa na kidiplomasia ili kutatua suala la nyuklia kwenye rasi ya Korea, Yuri Ushakov amesema.

Uhusiano wa biashara kati ya Urusi na Korea Kaskazini umeshuka kwa zaidi ya asilimia 56 mwaka 2018 kutokana na vikwazo vilivyowekewa serikali ya Korea Kaskazini, Yuri Ushakov ameongeza.

Kim ameondoka Pyongyang leo Jumatano asubuhi akitumia treni, shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA limeripoti.

Moscow inaabaini kwamba ni muhimu kwa Korea Kaskazini na Marekani kuendeleza mazungumzo kuhusu suala nyeti la mpango wa nyuklia wa kijeshi unaoendeshwa na Pyongyang.

Mwakilishi wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani amesema kuwa "Marekani na jumuiya ya kimataifa wana lengo moja - kitaka Korea Kaskazini kuachana moja kwa moja na mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia." Amesema mazungumzo yataendelea kati ya mjumbe maalum wa Korea Kaskazini, Stephen Biegun, na Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi ili kujaza kwa yale ambayo pande mbili hazijaafikiana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.